KARIBU KATIKA BLOG YETU AMBAPO UTAPATA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU TACEDE TANZANIA
<<<TACEDE NI ASASI ISIYO YA KISERIKALI ISIYO NA MASLAHI KIFEDHA YENYE KUTOA ELIMU YAKUJITAMBUA KATIKA JAMII>>>

TACEDE TANZANIA

TACEDE TANZANIA

Monday, September 4, 2017

FAHAMU KWA KIFUPI KUHUSU MAANA YA PETS (public expenditure and tracking system)

Pichani ni Ndugu Pai Nyanzandoba akitoa mchango wake kuhusu utekelezaji wa PETS, katika moja ya warsha zilizofanyika Morogora katika ukumbi wa Flomi Hotel, warsha hiyo iliendeshwa kwa muda wa siku tatu na kuhudhuliwa na wanachama mbalimbali wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kutoka mikoa sita. 

MAANA YA PETS (public expenditure and tracking system)
PETS (Public Expenditure Tracking Survey) ni mfumo au utaratibu wa wananchi  kufuatilia fedha za umma tangu zinapotolewa (Serikali kuu, n.k), kupitia halmashauri za (wilaya/miji/manispaa/jiji) hadi ngazi ya matumizi ya mwisho. Kwa maelezo mafupi ni WANANCHI KUFUATA PESA zao zilizoelekezo katika matumizi ya bajeti.

SIFA ZA PETS
 Ushirikishaji:  pamoja na Fuatilia pesa kuanzishwa na AZAKI, inatarajiwa kuwa mfumo huu utaendelezwa kwa ushirikiano baina ya AZAKI, TAMISEMI na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa

Kuanza Polepole na kwa Uangalifu: Kwa kuanzia PETS italenga kushughulikia mtiririko wa raslimali na kujaribu kuonyesha jinsi fedha zinavyotumika.  Hii itahusisha kushughulikia kwa ujumla kila chanzo cha mapato, na matumizi katika halmashauri

Kurahisha Utoaji Taarifa: kufuatia kuwapo juhudi za kutumia mfumo sanifu wa kompyuta wa PlanRep itakuwa rahisi kwa halmashauri kutoa taarifa

Kusaidia na si kukagua:  Kazi ya PETS si kuwa aina nyingine ya ukaguzi wa mahesabu. Bali, inakusudia kuufahamisha umma juu ya raslimali fedha zinazoletwa kwenye halmashauri, na kuwasaidia kuelewa jinsi mchakato wa bajeti na matumizi vinavyosimamiwa


FAIDA ZA PETS
   Itamuwezesha mwananchi kupata na kutumia taarifa za fedha.
  Itamsadia mwananchi  kuelewa uhusiano baina ya huduma zinazotolewa, fedha zinazotengwa na matumizi halisi.
Wananchi wanaweza kutumia taarifa zitokanazo na PETS Kujua iwapo pakacha linavuja mahali fulani  katika mtiririko (wapi na kwa kiasi gani). Mfano kulinganisha fedha iliyotolewa na serikali kuu, kiasi kilichopelekwa wilayani, na kiasi kilichopelekwa ngazi ya kijiji. (mapungufu na wapi yalipotokea )
  Kufahamu chanzo cha matatizo : mf upungufu wa vifaa vya kufundishia: je serikali haikutoa pesa? Je ugawaji ulikuwa mbovu?
Kujua sababu za Serikali kuu au Halmashauri kushindwa kutekeleza ahadi au mipango yake. Mfano Ahadi ya kujenga au kuboresha darasa au maabara. Fedha kutokupatikana kabisa? Au kupatika kwa hela pungufu?  
Kuhakiki thamani halisi ya fedha. Mfano Je Darasa iliyojengwa ina thamani ya Milioni 15? 

TACEDE itakuwa bega kwa bega kuhamasisha jamii kutumia mfumo huu wa ufatiliaji fedha za umma.





No comments:

Post a Comment