KARIBU KATIKA BLOG YETU AMBAPO UTAPATA TAARIFA MBALIMBALI ZINAZOHUSU TACEDE TANZANIA
<<<TACEDE NI ASASI ISIYO YA KISERIKALI ISIYO NA MASLAHI KIFEDHA YENYE KUTOA ELIMU YAKUJITAMBUA KATIKA JAMII>>>

TACEDE TANZANIA

TACEDE TANZANIA

Friday, October 6, 2017

JENGO LA TACEDE

Muonekano mpya wa nje wa jengo la ofisi ya Tabora Advocacy Centre for Development (TACEDE), ni muendelezo mzuri wa uboreshaji na utengenezeji wa ofisi yetu. Kwa mbele kunakisima cha maji ambapo ofisi hutoa huduma ya maji bure kwa jamii inayozunguka eneo la ofisi.

Monday, September 4, 2017

FAHAMU KWA KIFUPI KUHUSU MAANA YA PETS (public expenditure and tracking system)

Pichani ni Ndugu Pai Nyanzandoba akitoa mchango wake kuhusu utekelezaji wa PETS, katika moja ya warsha zilizofanyika Morogora katika ukumbi wa Flomi Hotel, warsha hiyo iliendeshwa kwa muda wa siku tatu na kuhudhuliwa na wanachama mbalimbali wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kutoka mikoa sita. 

MAANA YA PETS (public expenditure and tracking system)
PETS (Public Expenditure Tracking Survey) ni mfumo au utaratibu wa wananchi  kufuatilia fedha za umma tangu zinapotolewa (Serikali kuu, n.k), kupitia halmashauri za (wilaya/miji/manispaa/jiji) hadi ngazi ya matumizi ya mwisho. Kwa maelezo mafupi ni WANANCHI KUFUATA PESA zao zilizoelekezo katika matumizi ya bajeti.

SIFA ZA PETS
 Ushirikishaji:  pamoja na Fuatilia pesa kuanzishwa na AZAKI, inatarajiwa kuwa mfumo huu utaendelezwa kwa ushirikiano baina ya AZAKI, TAMISEMI na Mamlaka zote za Serikali za Mitaa

Kuanza Polepole na kwa Uangalifu: Kwa kuanzia PETS italenga kushughulikia mtiririko wa raslimali na kujaribu kuonyesha jinsi fedha zinavyotumika.  Hii itahusisha kushughulikia kwa ujumla kila chanzo cha mapato, na matumizi katika halmashauri

Kurahisha Utoaji Taarifa: kufuatia kuwapo juhudi za kutumia mfumo sanifu wa kompyuta wa PlanRep itakuwa rahisi kwa halmashauri kutoa taarifa

Kusaidia na si kukagua:  Kazi ya PETS si kuwa aina nyingine ya ukaguzi wa mahesabu. Bali, inakusudia kuufahamisha umma juu ya raslimali fedha zinazoletwa kwenye halmashauri, na kuwasaidia kuelewa jinsi mchakato wa bajeti na matumizi vinavyosimamiwa


FAIDA ZA PETS
   Itamuwezesha mwananchi kupata na kutumia taarifa za fedha.
  Itamsadia mwananchi  kuelewa uhusiano baina ya huduma zinazotolewa, fedha zinazotengwa na matumizi halisi.
Wananchi wanaweza kutumia taarifa zitokanazo na PETS Kujua iwapo pakacha linavuja mahali fulani  katika mtiririko (wapi na kwa kiasi gani). Mfano kulinganisha fedha iliyotolewa na serikali kuu, kiasi kilichopelekwa wilayani, na kiasi kilichopelekwa ngazi ya kijiji. (mapungufu na wapi yalipotokea )
  Kufahamu chanzo cha matatizo : mf upungufu wa vifaa vya kufundishia: je serikali haikutoa pesa? Je ugawaji ulikuwa mbovu?
Kujua sababu za Serikali kuu au Halmashauri kushindwa kutekeleza ahadi au mipango yake. Mfano Ahadi ya kujenga au kuboresha darasa au maabara. Fedha kutokupatikana kabisa? Au kupatika kwa hela pungufu?  
Kuhakiki thamani halisi ya fedha. Mfano Je Darasa iliyojengwa ina thamani ya Milioni 15? 

TACEDE itakuwa bega kwa bega kuhamasisha jamii kutumia mfumo huu wa ufatiliaji fedha za umma.





WANAMTANDAO WA ELIMU TANZANIA (TEN/MET)

TACEDE ni moja kati ya wanachama wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET), waliohudhulia warsha ya mafunzo ya Mfumo wa Ufatiliaji wa matumizi ya Fedha za umma - Public Expenditure Trackibg Systems (PETS), iliyofanyika mjini Morogoro. Mafunzo haya yalihudhuluwa na wa wakilishi wa asasi mbalimbali kutoka mikoa sita (6) ya kanda ya magharibi, mashariki na kati, yaani Tabora, Singida, Dodoma, Morogoro, Tanga na Dar-es-Salaamu.

Monday, July 10, 2017

Ni mafunzo ya jamii ya watu wa Igunga kwa mabinti waishio kwenye mazingira magumu na watoto wenye watoto, ni mafunzo juu ya life skills, sexuality, jinsia na kujilinda na maambukizi ya UKIMWI.

Thursday, June 22, 2017

JINSI YA KUVUA KONDOMU YA KIUME PINDI UMALIZAPO TENDO LA KUJAMIANA.

Wanasemina katika semina ya HIV PREVENTION iliyoandaliwa na TACEDE juu ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya UKIMWI, wakitoa mfano wa namna ya kutumia kondomu ya kiume, namna ya kuvaa na kuvua kondomu hiyo.

Mwanamke ndiye anayepaswa kumvua mwanaume kondomu wakati wa kumaliza tendo la kujamiana. Sababu za kimsingi ni kwamba; ile sehemu ya nje ya kondomu ndiyo iliyokua ndani mwa mwili wa mwanamke, hivyo kama sehemu hiyo ya ndani ilikuwa na michubuko ni rahisi sana damu kubaki sehemu ya nje ya kondomu hiyo, ikiwa kama mwanaume naye atakuwa na michubuko midogo au mikubwa kwenye mikono, halafu akashiki kuvua kondomu ile ni rahisi sana kupata maambukizi, Hivyo inashauriwa kiusalama zaidi, njia nzuri kuepuka hatari hiyo ni mwanamke mwenyewe amvue mwanaume kondomu.

Friday, June 16, 2017

SEMINA YA PREVENTION OF HIV

Godless akiongoza semina ya namna ya kuwaelimisha wafanyakazi wa kampuni za Kichina zinazoshughulika na ujenzi wa kipande cha barabara ya kutoka Dar mpaka Kigoma kupitia Tabora Manispaa juu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Semina hiyo ilifanyika kwa muda wa siku tatu iliyofanyika tarehe 12.06.2017 - 14.06.2017 katika ukumbi wa TDFT cheo Tabora,

SEMINA YA HIV PREVENTION

Baadhi ya washiriki wa semina ya HIV PREVENTION iliyotolewa na TACEDE katika ukumbi wa TDFT uliopo Cheo Mkoani Tabora, semina hii hutolewa kwa ajili ya kuwaelimisha wafanyakazi wote wafanyao kampuni za Kichina zinazohusika na ujenzi wa kipande cha barabara ya Dar mpaka Kigoma, kilichokatiza Tabora Manispaa.Kuhusiana na namna ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI